TANZANIA KUWASILISHA PENDEKEZO LA TSH TRIL 4 KATIKA COP29

 

TANZANIA KUWASILISHA PENDEKEZO LA TSH TRIL 4 KATIKA COP29

TANZANIA KUWASILISHA PENDEKEZO LA TSH TRIL 4 KATIKA COP29

TANZANIA
Tanzania inatarajiwa kuwasilisha pendekezo la miradi tisa yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1,433 (takriban shilingi trilioni 4)  katika Mkutano ujao wa Nchi Wanachama (COP29) unaotarajiwa kufanyika Kuanzia Novemba 11 hadi 22, 2024 mjini Baku, Azerbaijan.  
Mkutano wa kimataifa wa mazingira utatoa nafasi muhimu kwa nchi kuwasilisha mipango yao ya kitaifa ya hali ya hewa chini ya makubaliano ya Paris yenye msingi wa kuimarisha mwitikio wa pamoja dhidi ya tishio la mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuweka joto la kimataifa. 
Wajumbe wa nchi katika mkutano huo wataongozwa na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango kwa niaba ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Mwaka huu katika COP29 kutakuwa na mijadala itakayohusisha wajumbe wa nchi kwa lengo la kufikia dhamira ya pamoja na kuleta maelewano juu ya kuimarisha uhifadhi wa mazingira na hatua za tabia nchi.
Aidha, Tanzania itakuwa na banda katika mkutano huo kwa ajili ya kuonesha mipango mbalimbali ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo ipo katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchini.