SEKTA BINAFSI ZA TANZANIA NA UGANDA KUSHIRIKIANA
DAR ES SALAAM
Kamishna Mkuu wa Uganda nchini Tanzania, Balozi Kanali (Mst.) Fred Mwesigye, amesema kuwa ushirikiano wa Tanzania na Uganda unahusu zaidi miundombinu ili kukuza ushirikiano wa sekta binafsi kwa ukuaji endelevu.
Balozi Mwesigye ameyasema hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika Kongamano la Mtandao wa Mafuta na Gesi kati ya Uganda na Tanzania, lenye kaulimbiu ya ‘Driving Transformation in Uganda and Tanzania’s Energy Vision.
"Jukwaa hili linaonesha dhamira ya pamoja ya Uganda na Tanzania kutumia uwezo wa rasilimali zetu za mafuta na gesi kwa manufaa ya watu wetu”
Alisisitiza zaidi, “Ushirikiano wetu hauhusu miundombinu pekee, inahusu kujenga uhusiano wa sekta binafsi, kuunda nafasi za kazi, na kuhakikisha maendeleo endelevu."
Alibainisha kuwa ushirikiano wa Uganda na Tanzania, unaosimamiwa na Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki(EACOP¬), unawakilisha kielelezo cha utangamano wa kikanda na maendeleo ya pande zote mbili.
