MTANDAO WA BARABARA KM 109 KUFUNGULIWA
MANYARA
Serikali kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Manyara ina mpango wa kufungua barabara mpya zenye urefu Km. 109 katika Wilaya ya Mbulu, Simanjiro pamoja na Babati katika mwaka wa fedha 2024/2025.
Barabara zitakazofunguliwa ni zilizopo katika wilaya ya Mbulu (Km. 46), Simanjiro (Km. 41), pamoja na Babati (Km. 22).
Pamoja na ujenzi wa km 109 pia serikali itajumuisha ujenzi wa barabara za lami(Km. 11.7),changarawe (Km. 251.4) pamoja na matengenezo ya barabara za udongo (Km. 385) na ujenzi wa vivuko vipatavyo 104.
Licha ya kufungua kilomita hizo za barabara hali ya mtandao wa barabara katika maeneo mengi katika mkoa huo ni nzuri kwani unapitika katika kipindi chote cha mwaka.
