DKT SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA G20
BRAZIL
Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameshiriki mkutano wa siku mbili (tarehe 18 na 19) wa Mataifa 20 Tajiri Duniani, G20 jijini Rio de Janeiro, Brazil leo, na kupata nafasi ya kuwahutubia viongozi wa mataifa makubwa wanaounda muunganiko huo kama Marekani, Uingereza na China.
Katika hotuba yake, Mhe Rais Samia ametoa wito kwa mataifa tajiri duniani kutambua na kuzitumia fursa zilizopo barani Afrika, na kushiriki kutokomeza umasikini uliokithiri.
FAHAMU:- G20 inaundwa na Argentina, Australia, Brazili, Canada, China, Ufaransa, Ujerumani, India, Indonesia, Italia, Japan, Mexico, Urusi, Saudi Arabia, Afrika Kusini, Korea Kusini, Uturuki, Uingereza na Marekani.
