WANANCHI MUGOMA WAFURAHIA MRADI WA BARABARA

 

WANANCHI MUGOMA WAFURAHIA MRADI WA BARABARA

WANANCHI MUGOMA WAFURAHIA MRADI WA BARABARA

KAGERA
Wananchi wa Kata Mugoma Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera wameishukuru serikali kupitia Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kwa kurahisisha mawasiliano ya barabara ya Uzunguni na kuwapunguzia changamoto ya kutembea umbali mrefu kutoka Mgoma kwenda Ngara Mjini.
Mradi wa barabara ya Uzunguni umejengwa kwa kiwango cha lami kuanzia Oktoba 2023 hadi Juni kwa thamani ya Sh milioni 284 na kupunguza changamoto ya kutembea kwa muda mrefu .
Mchungaji Aneth Mzungu mkazi wa mtaa wa Uzunguni amesema kuwa moja ya changamoto kubwa iliyokuwepo katika barabara hiyo ni vyombo vya usafiri kushindwa kupanda mlima na kusababisha ajali, pamoja na wananchi wanaoishi mtaa huo kutofikishiwa huduma nyingine kwa urahisi kutokana na ubovu wa barabara hiyo
Haikuwa rahisi kupata bidhaa au serikali kuleta huduma au mtu kufungua biashara, barabara ilijaa tope wananchi walilazimika kufanya mzunguko mkubwa na kutumia gharama kubwa kuja mjini, lakini kwa sasa imerahisishwa na wanachi wanakatiza na huduma nyingi sana zimetufikia huku wengine wakijenga nyumba za kisasa kutokana na uwepo wa barabara nzuri, asema Mch.Aneth