TSH MIL 572.5 ZAPELEKA MAJI SERENGETI

 

TSH MIL 572.5 ZAPELEKA MAJI SERENGETI

TSH MIL 572.5 ZAPELEKA MAJI SERENGETI

MARA
Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha shilingi milioni 572.5 kwa ajili ya utekelezaji wa  mradi wa maji wa kijiji cha Nyamihuru wilayani Serengeti Mkoani Mara.
Mradi huu umeanza kutekelezwa mwezi Aprili 2024 ambapo tayari umefikia 75% ya utekelezaji  na unahusisha uwekaji wa nyumba ya mashine na miundombinu ya umeme kwa ajili ya kusukuma maji.
Shughuli nyingine zinazofanyika ni kujenga mtandao wa maji wenye urefu wa kilomita 9.92,tenki la maji lenye ujazo wa lita 200,000, vibanda tisa vya maji na uzio wa chanzo cha maji.