SERIKALI KUANZA UJENZI WA SONGEA BYPASS

 

SERIKALI KUANZA UJENZI WA SONGEA BYPASS

SERIKALI KUANZA UJENZI WA SONGEA BYPASS 

RUVUMA
Serikali imedhamiria kuondoa msongamano wa magari makubwa katikati ya Manispaa ya Songea kwa kujenga barabara ya mchepuo (Songea Bypass) yenye urefu wa kilometa 16 ambapo utekelezaji huo utaenda sambamba na ujenzi barabara ya Songea - Njombe (km 100).
Mwezi huu Oktoba 2024, Serikali itasaini mkataba wa kuanza utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Lukuyufusi  - Lipapasi - Mkenda (km 60) kwa kiwango cha lami ili kuunganisha Mkoa wa Ruvuma na nchi jirani ya Msumbiji.
Aidha serikali kupitia Wizara ya Ujenzi ipo katika hatua ya kumpata mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Daraja la Mitomoni lenye urefu wa mita 80 litakalounganisha Wilaya ya Songea Vijijini na Wilaya ya Nyasa.