VIJIJI 4,041 VYAFIKISHIWA HUDUMA YA MAWASILIANO

 

VIJIJI 4,041 VYAFIKISHIWA HUDUMA YA MAWASILIANO

VIJIJI 4,041 VYAFIKISHIWA HUDUMA YA MAWASILIANO

Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imefikisha huduma ya mawasiliano ya simu katika vijiji 4,041 vilivyo katika Kata 1,399 kwa kujenga minara 1,532.(Hii ni kwa mujibu wa UCSAF katika maonesho ya kimataifa ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi maarufu kama NaneNane yaliyofanyika kitaifa kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti, 2024 katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma).
Hivi sasa Serikali kupitia UCSAF inatekeleza mradi wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano ya simu vijijini, inayojengwa katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara, ambapo jumla ya Kata 713 zenye jumla ya vijiji 1,407 zinafikiwa kupitia mradi huu.
Serikali inawekeza katika kuboresha mawasiliano kwa kuwa ni nyenzo inayowezesha wakulima kupokea taarifa muhimu kuhusu masuala mbalimbali kama vile taarifa za hali ya hewa na mbinu bora za kilimo.