BAJETI MATENGENEZO YA BARABARA DODOMA YAFIKIA TSH BIL 66.2
DODOMA
Bajeti ya matengenezo na ukarabati wa barabara na madaraja kwa mkoa wa Dodoma imeongezeka kutoka Shilingi bilioni 12.7 mwaka 2020/2021 hadi kufikia Shilingi bilioni 66. 2 mwaka 2023/24.
Ongezeko la bajeti limesaidia kuimarika kwa ubora wa mtandao wa barabara za lami kutoka Km 171.29 hadi Km 309.71, barabara za changarawe kutoka Km 1,258.65 hadi Km 1,827.5, madaraja 19, maboksi kalavati 45
Mitaro yenye urefu wa mita 73,822.24 imejengwa, taa za barabarani 470 zimesimikwa, barabara mpya zenye urefu wa Km 544.60 zimefunguliwa ambazo hazikuwepo kabisa
Aidha serikali kupitia Wakala wa barabara umetekeleza miradi ya kielelezo ujenzi wa barabara za lami Mji wa Serikali Mtumba Km 12.6, barabara ya lami Mwanga-Kisasa-Medeli Km 10.7, barabara ya lami Swaswa-Mpamaa-Arusha Road Jct Km 8.2, barabara ya lami ya mzunguko Mlimwa Km 1.55
