BARABARA KAZILAMBWA – CHAGU (KM 36) YAJENGWA
TABORA
Serikali kupitia wizara ya Ujenzi imekamilisha ujenzi wa barabara kilomita 36 kiwango cha lami Kazilambwa – Chagu) katika kijiji cha Ugansa mkoani Tabora huku ikiendelea na ujenzi kipande cha Ugansa-Usinge (Km 7.41).
Ujenzi wa barabara ya Kazilambwa-Chagu (Km 36) na Ugansa-Usinge (Km 7.41) ni muendelezo wa juhudi za Serikali kuifungua nchi katika kuboresha huduma za usafiri na uchukuzi na hivyo kuleta tija kwa wananchi.
Aidha ujenzi wa barabara ya Kazilambwa-Chagu (Km 36) ni sehemu ya barabara ya Kaliua-Malagarasi-Ilunde Km 156 ambapo kukamilika kwake kutaunganisha mkoa wa Tabora na Kigoma kwa lami.
