UCHUMI WA TANZANIA WAIBEBA (SADC)
DAR ES SALAAM.
Tanzania imekuwa kitovu cha uwekezaji na kusababisha ukuaji wa uchumi katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka 4.7% mwaka 2022 hadi kufikia 5.0% mwaka 2023 huku matarajio ya uchumi wa Tanzania kwa mwaka 2024 yakiwa ni 5.5%
Kuelekea hatua za ukuaji wa uchumi, serikali imeendelea kufanya maboresho ya sera na kanuni za uwekezaji (Rejea sheria ya uwekezaji ya mwaka 2022) ili kujibu changamoto za uwekezaji na wafanyabiashara ili waweze kulipa kodi kwa hiari na kuiwezesha serikali kutekeleza mahitaji kwa umma.
Serikali imekuwa ikishirikiana na sekta binafsi kufanya makusanyo ya mapato yaliyotekelezwa kutokana na miradi mbalimbali ya maendeleo na hiyo ni pamoja na kudhibiti mfumuko wa bei uliofikia 3.2% kwa mwezi Julai hadi Desemba 2023 kiwango ambacho kipo ndani ya lengo la kati ya asilimia 3 hadi 7.
Aidha Makusanyo ya Sh trilioni 22.6 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 yalipelekea kuongezwa kwa bajeti kuu ya serikali kutoka Shilingi trilioni 36 mwaka 2021/2022 hadi Sh trilioni 44.4 mwaka 2023/2024 ambazo zimesaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo reli ya kisasa ya SGR ambayo imefanyiwa majaribio ya mafanikio hivi karibuni, ukarabati wa miundombinu ya bahari na maziwa makuu, pamoja na asilimia 79 ya vijijini kufikiwa na huduma ya maji.
