TSH BIL 8 ZIMEENDA KWENYE MIRADI 16 YA MAJI SIMIYU.

 

TSH BIL 8 ZIMEENDA KWENYE MIRADI 16 YA MAJI SIMIYU.

TSH BIL 8 ZIMEENDA KWENYE MIRADI 16 YA MAJI SIMIYU.

SIMIYU
Serikali kupitia Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Simiyu imeingia mikataba yenye thamani ya Sh bilioni 8 na wakandarasi 14 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji 16 mkoani humo ambayo itatekelezwa katika Wilaya za Meatu, Busega pamoja na Bariadi.
Miradi hiyo ikikamilika ujenzi wake itaongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji mkoani humo ambapo kwa sasa upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu ni 71.0%, kutoka 68.20% mwaka 2022.
USICHOKIJUA:- Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Mkoa wa Simiyu umeidhinishiwa jumla ya Sh bilioni 31.8 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji 32 kwenye wilaya zote tano, kati ya hiyo miradi 16 ndiyo imesainiwa hivi karibuni na miradi yote 32 ikimalika itaifanya Mkoa wa Simiyu kufikisha 81% ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.