TSH MIL 776.83 KUPANUA ZAHANATI NKOME

 

TSH MIL 776.83  KUPANUA ZAHANATI NKOME

TSH MIL 776.83  KUPANUA ZAHANATI NKOME

GEITA
Serikali imetenga takribani Sh milioni 776.83 kwa ajili ya upanuzi wa zahanati ya kijiji na kata ya Nkome katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mkoani Geita hatua itakayoiwezesha zahanti hiyo kupanda hadhi na  kuwa kituo cha afya.
Upanuzi wa zahanati hiyo kuwa kituo cha afya unahusisha ujenzi wa majengo matatu ya (jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD), Jengo la Maabara na Jengo la Wodi ya Wazazi) 
Ujenzi huu unatekelezwa kwa awamu mbili, na kusimamiwa na wakandarasi wawili tofauti akiwemo Tujenge Pamoja Afrika kwa mkataba wa Sh milioni 540.69 kwa hatua ya msingi na kupiga lipu na kampuni ya GIPCO Construction Limited kwa mkataba wa Sh milioni 236 .76 kwa hatua ya ukamilishaji na kufanya jumla ya mkataba kuwa Sh milioni 776.83.