UPANUZI WA BANDARI YA MWANZA, BUKOBA WAENDELEA
MWANZA
Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema miradi ya upanuzi wa bandari za Mwanza na Bukoba unaendelea vizuri na utaanza kazi zake za kawaida mapema mwakani.
Ujenzi na upanuzi huo unahusisha Bandari tatu Mwanza Kaskazini,ambayo ujenzi umefikia 40%, Kemondo 75% na Bukoba,ambayo pia imekamilika kwa 73%.
Miradi yote mitatu inagharimu takriban shilingi bilioni 60 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya uboreshaji na upanuzi wa bandari hizo,kati ya sita zilizopo Ziwa Victoria na utatekelezwa kwa muda wa miezi 18.
