MARA WAPOKEA MAGARI KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI

 

MARA WAPOKEA MAGARI KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI

MARA WAPOKEA MAGARI KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI

MARA 
Mkoa wa MARA umepokea magari mawili kutoka serikali kuu yenye thamani ya shilingi  milioni  410  kwa ajili ya kuharakisha miradi ya maji ambayo ni ngumu kufikiwa katika wilaya za Serengeti na Tarime inayotekelezwa kupitia Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa).
Miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa maji wa Nyanungu wa Tarime wenye thamani ya shilingi bilioni 1.4  ulioanza Aprili mwaka huu na unatarajiwa kukamilika mwezi  Novemba 2024.
Mradi huo unahusisha ujenzi wa matanki mawili ya maji yenye ujazo wa mita za ujazo 150,kisima chenye uwezo wa kuchukua lita 135,000 na mtandao wa maji wa kilomita 37,pamoja na vituo 22 vya kusambaza maji au vioski.
Mradi wa Nyanungu ambao kwa sasa umekamilika kwa asilimia 65, unatarajiwa kuwanufaisha wananchi 11,195 katika vijiji vya Nyandage,Mangucha, Kegonga na Nyamombara.
Mradi mwingine wa Tarime wa Kimusi, unagharimu zaidi ya 1.06bn/- na ulianza Mei mwaka  2023 na Unatarajiwa kukamilika Desemba  2024 na utawanufaisha takriban watu 11,230 katika vijiji vya Kimusi, Gwitare na Ntagacha.