AUSTRALIA KINARA UWEKEZAJI MADINI TANZANIA

 

AUSTRALIA KINARA UWEKEZAJI MADINI TANZANIA

AUSTRALIA KINARA UWEKEZAJI MADINI TANZANIA

PERTH,AUSTRALIA
Tanzania imetajwa kuwa nchi kinara kwa Bara la Afrika ambayo kampuni za Madini za Australia zimewekeza kwa asilimia 21% ya uwekezaji wote wa kwenye Sekta ya Madini.
Hayo yameelezwa  Perth, Australia wakati wa mkutano wa Africa DownUnder(ADU) uliowashirikisha wadau wa madini kutoka Australia na Nchi za Bara la Afrika.
Kwa miaka miwili iliyopita biashara baina ya Kampuni za Madini za Australia na Serikali ya Tanzania ina thamani ya zaidi ya Shilingi Trilioni Kumi na hivyo utekelezaji wake utasaidia kuongeza mapato ya nchi,kuongeza nafasi za ajira,ushiriki wa watanzania(Local Content) na kuchochea ukuaji wa sekta ya madini.
Watendaji wa Kampuni za Chief , Walkabout Resources, Peak Rare Earths, Black Rock Mining na Eco Graf kwa pamoja wameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na hivyo kuvutia uwekezaji huu mkubwa nchini ambao utachochea kukuaji wa kasi wa uchumi wa Tanzania.