TSH BIL 11 KUKARABATI IMS ZANZIBAR

 

TSH BIL 11 KUKARABATI IMS  ZANZIBAR

TSH BIL 11 KUKARABATI IMS  ZANZIBAR

DAR ES SALAAM
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinaanza mradi kabambe wa kukarabati Taasisi ya Sayansi ya Bahari (IMS) iliyopo Buyu, Zanzibar,kwa uwekezaji mkubwa wa shilingi bilioni 11.
Mradi huo unafadhiliwa na Mpango wa Benki ya Dunia wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), unaolenga kuimarisha uwezo wa utafiti na kukuza mbinu endelevu za uvuvi katika kanda.
Ukarabati huo utafanya vifaa kuwa vya kisasa,kuandaa maabara na kutoa rasilimali kwa utafiti wa hali ya juu katika mifumo ikolojia ya baharini na uvuvi.
Kituo hicho kitajumuisha kumbi mbili za mihadhara zenye uwezo wa kuchukua takriban wanafunzi 216, maabara tano,vyumba vinne vya madarasa na ukumbi wa mikutano.