BARABARA BIHARAMULO YAZINDULIWA RASMI
KAGERA
Mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kilometa 0.75 wenye thamani ya Sh milioni 423 unaolenga kuboresha mazingira na kukuza uchumi katika mji mdogo wa Biharamulo mkoani Kagera umekamilika na umezinduliwa rasmi tayari kwa kuanza kutumika.
Utekelezaji wa barabara hiyo umeboresha mazingira ya mji na kufanya mji kuwa safi na kuongeza kasi ya wananchi kutumia fursa zaidi katika kuingiza mazao kwani hakutakuwa na changamoto ya kukwama kwa usafiri.
Mradi huo umetekelezwa kwa kipindi cha miezi sita tangu Oktoba 2023 hadi April 2024 kutoka kwenye fedha za mfuko wa jimbo na baada ya mradi huo kukamilika wananchi wameanza kunufaika na wanaendelea na kufanyabiashara zao kwa saa 24.