TPA KANDA YA ZIWA YAHUDUMIA TANI 80,999

 

TPA KANDA YA ZIWA YAHUDUMIA TANI 80,999

TPA KANDA YA ZIWA YAHUDUMIA TANI 80,999

MWANZA
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Kanda ya Ziwa imehudumia tani 80,999 za mizigo katika robo ya kwanza, kati ya tani 335,096 zilizopangwa kwa mwaka huu wa fedha ikilinganishwa na mwaka jana ambapo bandari iliweza kufikia tani 236,274 kati ya tani 310,000 zilizolengwa.
Lengo la mwaka jana  halikufikiwa kutokana na ukarabati mkubwa wa meli tatu za mizigo katika Ziwa Victoria ambazo ni MV Umoja, MV Kaawa na MV Pamba.
Meli hizo za mizigo kwa sasa zimerejea kufanya kazi, na mizigo inatarajiwa kuongezeka zaidi kutokana na upanuzi mkubwa unaoendelea na ujenzi wa bandari za Mwanza Kaskazini, Bukoba na Kemondo.
Kuimarishwa huku kwa uwezo wa kibiashara ni matokeo ya huduma bora za ugavi, kupunguza gharama na muda wa usafirishaji wa bidhaa, ambayo ni muhimu kwa kudumisha ushindani katika soko la kimataifa.
Aidha kuongezeka kwa ushughulikiaji wa mizigo kunatokana na uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya bandari na vifaa vya kisasa vinavyohusika na usafirishaji, ambavyo vina mchango mkubwa katika kuimarisha mitandao ya usafirishaji, ikiwa ni pamoja na barabara na reli.