DKT SAMIA AAGIZA KANISA KATOLIKI ARUSHA WAREJESHEWE ENEO NA TSH. MIL. 500
ARUSHA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amerejesha eneo la Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, ambalo lilichukuliwa na Halmashauri ya Jiji la Arusha na kuagiza fedha Sh500 milioni zilizokuwa zimetolewa na Kanisa kwa ajili ya kununua tena eneo hilo na warejeshewe.
Agizo hilo lilitolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya ofisi ya mkuu wa mkoa Arusha kuwasilisha maombi hayo ya kanisa wakati wa kuhitimisha ziara yake mkoani humo.
Mhe. Mchengerwa amesema Rais ameelekeza Uongozi wa Mkoa wa Arusha na Halmashauri ya Jiji la arusha, kurejesha eneo hilo kwa kanisa mara moja pamoja na fedha hizo walizokuwa wametoa kwa ajili ya kununua eneo lao wenyewe.
“Rais amenielekeza eneo hilo lirejeshwe kwa kanisa mara moja na Shilingi milioni 500 ambayo mliichukua kwa kanisa zirejeshwe mara moja na hili niwaelekeze mkoa kulisimamia kuhakikisha fedha hizi zinarudi kwa kanisa kama ambavyo namna mlizuchukua kutoka kanisani,”alisema Mh Mchengerwa.
