RUVUMA WANA MAGARI MAPYA 15 YA KUBEBEA WAGONJWA
RUVUMA
Serikali imepeleka magari 15 mapya ya kubebea wagonjwa (Ambulance) katika Mkoa wa Ruvuma na kuufanya mkoa huo kuwa na jumla ya magari 21 ya kubebea wagonjwa hatua ambayo imeimarisha zaidi huduma za rufaa za wagonjwa hasa mama na mtoto (M-mama).
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto lengo likiwa ni kupunguza na kumaliza tatizo la vifo vinavyotokana na uzazi na vifo vya Watoto wachanga vinavyozuilika.
FAHAMU:- Mfumo wa M-mama Mkoani Ruvuma ulizinduliwa Mei 2023,hadi sasa umewezesha kusafirisha jumla ya wagonjwa 1,938 kati yao akinamama wajawazito 1,664 na Watoto wachanga 274.
