BARABARA INAYOUNGANISHA VIJIJI 68 MUSOMA KUJENGWA
MARA
Barabara pekee inayounganisha vijiji vyote 68 Musoma vijijini yenye urefu wa km 92 (Musoma-Makojo-Busekera) inajengwa wa kiwango cha lami hatua ambayo itarahisisa itaimarisha kwa kiasi kikubwa shughuli za kiuchumi na kijamii Musoma Vijijini na pamoja na urahisi wa upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na matibabu.
Hadi hivi sasa ujenzi kutoka Kijiji cha Kusenyi hadi Kijiji cha Suguti umeanza huku kilomita 40 akitafutwa mzabuni kwa ajili ya atuanza utekeleaji.
Mradi huu unaendana na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2020-2025, ambayo inalenga katika kukuza uchumi wa kisasa, jumuishi, shirikishi na wa ushindani unaozingatia ujenzi wa viwanda, huduma za kiuchumi na miundombinu wezeshi kama barabara.
Pia inasaidia Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP III) kuanzia 2021/22 hadi 2025/26, ambao unasisitiza kufungua miundombinu ya usafiri ili kukuza ukuaji. Chini ya Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano, serikali inalenga kujenga kilomita 6,006 za barabara za lami kote nchini.
