NJOMBE KUJENGEWA KAMPASI YA UDOM

 

NJOMBE KUJENGEWA KAMPASI YA UDOM

NJOMBE KUJENGEWA KAMPASI YA UDOM

NJOMBE
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itaanza ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Mkoani Njombe ujenzi ambao utatekelezwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) ambayo itakuwa Taasisi ya Kwanza ya Elimu ya Juu katika mkoa huo.
Ujenzi wa Kampasi hiyo utaanza Disemba 2024, utagharimu shilingi bilioni 20 na ujenzi ukikamilika chuo kinatarajiwa kuchukua wanafunzi 1000 na kitaanza kwa kutoa kozi za stashahada na shahada za ujuzi katika fani za kilimo, TEHAMA, Misitu pamoja na mazao yake na zingine zinazoendana na shughuli za kiuchumi za Mkoa wa Njombe.