TSH BIL 29 MABORESHO KIWANJA CHA NDEGE MWANZA
MWANZA
Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 29 kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la abiria katika kiwanja cha ndege cha Mwanza.
Kiasi hicho cha fedha kitawezesha ukamilishaji wa maeneo ya biashara nje ya jengo, ujenzi wa maegesho ya magari mia tatu, ujenzi wa barabara ya kuingia na kutoka kwenge jengo la abiria, ujenzi wa barabara kiunganishi kati ya jengo hilo na maegesho ya ndege na ujenzi wa uzio wa usalama kuzunguka jengo lote.
