FAHAMU BARABARA ZINAZOJENGWA IRINGA KWA SASA

 

FAHAMU BARABARA ZINAZOJENGWA IRINGA KWA SASA

FAHAMU BARABARA ZINAZOJENGWA IRINGA KWA SASA

IRINGA 
Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inaendelea na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Wenda-Mgama Km 19 na Mtili-Ifwagi Km 14 katika Wilaya ya Iringa na Mufindi mkoani Iringa ambapo Ujenzi wa barabara hizo unategemea kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2025.
Barabara hizo zinazojengwa chini ya Mradi wa Uboreshaji wa Barabara Vijijini kwa Ushirikishaji wa Jamii na Ufunguaji wa Fursa za Kijamii na Kiuchumi (RISE) zinalenga kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
FAHAMU:- Kwa sasa TARURA kupitia mradi RISE inatekelza miradi ya ujenzi wa barabara katika Mikoa ya Iringa, Geita, Tanga na Lindi.