JE UNAFAHAMU KWAMBA TZ INA MADINI YA MKAKATI

 

JE UNAFAHAMU KWAMBA TZ INA MADINI YA MKAKATI

JE UNAFAHAMU KWAMBA TZ INA MADINI YA MKAKATI

DODOMA
Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizobarikiwa kuwa na madini mkakati ambayo uhitaji wake ni mkubwa kwenye nishati safi na salama na teknolojia nyingine za kisasa duniani
Madini hayo ya mkakati yanayopatikana nchini ni pamoja na lithium, cobalt, nikeli, shaba, aluminium, zinki, kinywe na rare earth elements (REE).
 Aidha, uhitaji huu unatokana na utekelezaji wa azimio la pamoja la dunia la kupunguza hewa ya ukaa ifikapo 2050 (Net Zero Emission). 
Kutokana na uwepo wa madini hayo na ili yalete manufaa kwa nchi yetu serikali kupitia Wizara ya madini imeandaa mkakati unaolenga kuhakikisha madini hayo yanaongezwa thamani hapa nchini ikiwemo kuzalisha bidhaa zinazohitajika katika soko kama vile betri za magari ya umeme na hivyo kuongeza manufaa kwa nchi ikiwemo kuongeza mapato ya Serikali na ajira kwa watanzania.