2023/24 UWEKEZAJI ILIIDHINISHIWA TSH BIL 126+
TANZANIA
Katika mwaka 2023/24, Mafungu matatu (3) ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji yaliidhinishiwa zaidi ya shilingi bilioni 126 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo.
Kati ya fedha hizo, kiasi cha shilingi bilioni 15.61 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi na shilingi bilioni 79.90 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi bilioni 30.69 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
