TSH MIL 540 ZAFIKISHA MAJI SANGE, PANGANI

 

TSH MIL 540 ZAFIKISHA MAJI SANGE, PANGANI

TSH MIL 540 ZAFIKISHA MAJI SANGE, PANGANI

TANGA
Serikali kupitia wizara ya maji chini ya mradi wa lipa kwa matokeo (PforR) katika Sekta ya Maji imetumia kiasi cha shilingi milioni 540 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maji Sange wilayani Pangani Mkoani Tanga ambapo utekelezaji wake ni asilimia 90 .
Ujenzi wa mradi huo umehusisha tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 50000,ujenzi wa nyumba ya mtambo wa kusukuma maji na ujenzi wa vituo vya umma vya kuchotea maji 13 na ulazaji wa mabomba zaidi ya Mita 9,900.
Wilaya ya Pangani kwa sasa hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama imefikia asilimia 92 na wananchi wameshukuru serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kufanikisha huduma ya maji kwa watu wote.