MAKUSANYO YA KODI YAONGEZEKA NCHINI
DAR ES SALAAM
Maamuzi ya serikali ya kuimarisha mifumo ya ukusanyaji kodi nchini yameanza kuleta mafanikio baada ya kuongezeka kwa makusanyo ya kodi kutoka wastani wa shilingi milioni 850 kwa mwezi mwaka 2015 hadi bilioni 2 kwa mwezi mwaka 2022/23.
Aidha kwa takwimu ya makusanyo ya kodi kwa mwezi uliopita (septemba 2024)Nchi imeweza kukusanya zaidi ya shilingi trilioni 3
Hatua ambazo serikali imezichukua ni pamoja na kuimarisha mazingira ya kufanya biashara nchini,kufuta baadhi ya tozo, kuimarisha utendaji kwenye idara za serikali,wakala na taasisi mbalimbali za serikali.