BARABARA KYERWA SEKONDARI YAFIKIA 96%
KAGERA
Mradi wa ujenzi barabara ya Kyerwa Sekondari wenye thamani ya Sh milioni 474 kilomita moja kwa kiwango cha lami Mkoani Kagera umefikia asilimia 96 ya ukamilikaji wake ambapo Novemba mwaka huu utamalizika.
Barabara hiyo imekuwa muhimu kwani baada ya kuanza kwa mradi tayari wawekezaji wamejenga viwanda katika eneo hilo kuna huduma ya shule na wananchi wamevutiwa kujenga makazi.
Kwa kipindi cha miaka mitatu kuna ongezeko la barabara za lami makao makuu ya wilaya hiyo mpya mpaka kilometa 5 na serikali inaendelea kuongeza jitihada za kutengeneza barabara .
