MAKAO MAKUU YA CPA KUJENGWA DODOMA
ARUSHA
MAKAO Makuu ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA) Kanda ya Afrika yanatarajiwa kujengwa mjini Dodoma huku maandalizi ya kuanza kwake yakiendelea(Hii ni kwamujibu wa Salome Makamba, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA) Kanda ya Afrika kupitia kwa Mkutano Mkuu wa 53 wa Mwaka wa CPA Kanda ya Afrika uliofanyika Arusha mwishoni mwa wiki).
Ujenzi huo unakadiriwa kugharimu zaidi ya dola za kimarekani milioni 30 (takribani shilingi 81,900,000,000).
Aidha wakati wa kuhitimisha mkutano huo, zaidi ya maazimio 20 yaliwasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maazimio, Bi Nontembeko Boyce, ambaye pia ni Spika wa Bunge la KwaZulu Natal nchini Afrika Kusini. Maazimio haya yalipitishwa na wajumbe wote.
Maazimio hayo yalijumuisha kuzihimiza serikali za Afrika kutekeleza mageuzi ya sera ambayo yanajumuisha mikakati ya mabadiliko ya tabianchi katika ngazi zote za utawala, kuhimiza ushirikishwaji wa jamii kupitia kampeni za uhamasishaji wa umma na kuhimiza mipango ya kuvuka mipaka ili kukabiliana na changamoto za pamoja za hali ya hewa kama vile jangwa, ukame na mafuriko na mengineyo
