KAHAWA YA TANZANIA , HAISHIKIKI JAPAN.

 

KAHAWA YA TANZANIA , HAISHIKIKI JAPAN.

KAHAWA YA TANZANIA , HAISHIKIKI JAPAN.

JAPAN
Balozi wa Tanzania nchini Japan, Baraka Luvanda, amesema kuwa Japan inaagiza wastani wa tani 15,000 za kahawa kwa mwaka huku kahawa ya Tanzania ikipendwa zaidi kutokana na ubora wake.
Kahawa ya Tanzania ndiyo chaguo bora zaidi miongoni mwa watumiaji wa Japan kwa unywaji wao wa kila siku, huku asilimia 70 wakipendelea chapa za Tanzania kuliko nyinginezo.
Kufuatia hatua hiyo, balozi Luvanda amewataka wakulima kote nchini kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazopatikana katika soko la Japan.
"Nawaomba Watanzania wenzangu wachangamkie fursa hii," amesema.
FAHAMU:- Kwa mujibu wa takwimu za COMTRADE za Umoja wa Mataifa, mauzo ya Tanzania kwenda Japan yalifikia takriban dola za Marekani milioni 68 (kama  shilingi bilioni 186/-) mwaka 2023, huku uagizaji kutoka Japan ukiwa na jumla ya dola za Marekani milioni 650 (takribani shilingi trilioni 1.8 ).