TSH BIL 140 KUIMARISHA MIUNDOMBINU MKOANI LINDI

 

TSH BIL 140 KUIMARISHA MIUNDOMBINU MKOANI LINDI

TSH BIL 140 KUIMARISHA MIUNDOMBINU MKOANI LINDI

LINDI
Serikali imesaini mikataba mitano kwa ajili ya ujenzi wa Madaraja 13 katika sehemu za barabara zilizoathiriwa na Mvua za El-Nino na Kimbunga Hidaya mnamp mwezi Februari hadi Mei 2024 katika Mkoa wa Lindi ambapo jumla ya Tsh. Bilioni 140 zitatumika.
Baadhi ya maeneo yatakayofanyiwa matengenezo ni daraja la mita 60 lililopo eneo la Somanga mtama, daraja la mita 40 katika eneo la Kipwata, daraja la mita 40 katika eneo la Mikereng'ende,daraja la mita 60 Matandu na daraja la Mbwenkuru na maeneo mengine.
Miradi hiyo itatekelezwa ndani ya kipindi cha miezi 36 tangu kusainiwa kwa mkataba Mwezi  Oktoba 2024.