BARABARA YA RUANGWA – NANGANGA (KM 53.2) KUKAMILIKA FEB. 2025
LINDI
Ujenzi wa barabara ya Ruangwa – Nanganga (Km 53.2) kwa kiwango cha lami umefikia 81% huku ukitarajiwa kukamilika Februari 2025.
Katika hatua nyingine Serikali ipo katika hatua za mwisho kupata wakandarasi watakaojenga madaraja yaliyoathiriwa na mvua kubwa ziliyonyesha mwaka huu katika barabara ya Mingoyo – Dar es Salaam ili kuyajenga katika ubora utakaoweza kuruhusu maji kupita kwa urahisi na kulinda barabara hiyo.
