MRADI WA MAJI BYEJU WAFIKIA 90%
KAGERA
Mradi wa maji Byeju wilayani Missenyi mkoani Kagera wenye thamani ya Sh bilioni 2.4,ambao unatarajia kunufaisha zaidi ya wananchi 26,000 umefikia utekelezaji wa asilimia 90.
Mkataba wa ujenzi wa mradi huu ulisainiwa Octoba,2023 na mkandarasi alianza kutekeleza mradi huo Desemba 2023 na unatarajia kukamilika hivi karibuni.
Kukamilika kwa mradi huo kutaongeza nguvu ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa Byeju wilayani Misenyi Mkoani Kagera.
