MRADI WA MAJI GEITA KUFANYIWA MAJARIBIO 2025
GEITA
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita (GEUWASA) imeeleza ifikapo Juni 2025 mradi wa maji wa miji 28 wilayani Geita utafanyiwa majaribio kabla ya kukabidhiwa rasmi Desemba 2025.
Mradi huo wilayani Geita unatekelezwa kwa gharama ya Sh bilioni 124 ukihusisha ujenzi wa matenki matano ya maji, kituo cha kupokea maji, kituo cha kutibu maji na usambazaji wa mabomba.
Huu ni mradi mkubwa ambao utaenda kuleta lita milioni 45 kwa siku kwa mji wa Geita kwa wakazi wote wa kata 13, pamoja na vijiji 19 vitakavyopitiwa na bomba kubwa la maji kutoka ziwani.
Aidha Kwa sasa mahitaji ya maji mjini Geita ni lita milioni 22 kwa wastani lakini mradi huu utazalisha lita milioni 45 kwa hiyo utazalisha mara mbili ya mahitaji ya sasa hivi.