MHE.RAIS MWINYI KUMUWAKILISHA DKT SAMIA KWENYE TROIKA SADC

 

MHE.RAIS MWINYI KUMUWAKILISHA DKT SAMIA KWENYE TROIKA SADC

MHE.RAIS MWINYI KUMUWAKILISHA DKT SAMIA KWENYE TROIKA SADC

TANZANIA
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi  anatarajiwa kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa asasi ya siasa, ulinzi na usalama wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa dharura wa wakuu wa nchi na serikali wa SADC utakaofanyika tarehe 20 Novemba 2024 jijini Harare, Zimbabwe.
Pamoja na ushiriki huo Dkt Mwinyi ataongoza pia mkutano wa dharura wa wakuu wa nchi na serikali wa utatu wa asasi ya siasa,ulinzi na usalama utakaofanyika siku hiyohiyo ya tarehe 20 Novemba 2024.