TSH BIL 5.3 KWENYE MABADILIKO YA TABIANCHI
ZANZIBAR
Kiasi cha shilingi bilioni 5.3 zimetolewa kwa kipindi cha miaka mitatu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya inayohusu mazingira na mabadiliko ya Tabianchi Tanzania bara na visiwani (Kutokana na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis).
Serikali imekuwa ikipokea fedha kutoka kwenye Mifuko ya Kimataifa ya Mazingira na mabadiliko ya Tabianchi ikiwemo Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) na Mfuko wa Mabadiliko ya tabianchi (GCF).
Fedha hizo zinazotolewa zimekuwa zikitumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ya hifadhi ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi katika pande zote mbili za Muungano na kwa kiasi kikubwa zimesaidia kutekeleza Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula kwenye maeneo mbalimbali nchini.