TANZANIA & CHINA ZAREKODI TSHS TRIL 30 ZA FDIs

 

TANZANIA & CHINA  ZAREKODI TSHS TRIL 30 ZA FDIs

TANZANIA & CHINA  ZAREKODI TSHS TRIL 30 ZA FDIs

TANZANIA
Tanzania imerekodi kwa kiasi kikubwa zaidi ya dola za Marekani bilioni 11 (kama shilingi trilioni 30/-) kama Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Nje (FDIs) kutoka China katika miaka 60 ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili - hii ikiwa ni pamoja na kuimarishwa kwa ushirikiano wa kisiasa na kijamii na kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.
Kupitia Kongamano la Maendeleo ya Pamoja kati ya China na Tanzania lililofanyika jijini Dar es Salaam,  taarifa utoka wizara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji imesema mafanikio hayo yanatokana na uhusiano mzuri wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
Taarifa hiyo imefafanua zaidi kuwa uhusiano mkubwa kati ya Tanzania na China umesababisha China kuwa mshirika mkuu wa biashara wa Tanzania na chanzo cha FDIs. 
Kongamano hilo ambalo liliandaliwa kwa pamoja na serikali ya Tanzania na Ubalozi wa China nchini Tanzania lililenga kuangazia ushirikiano wa kidiplomasia wa nchi hizo mbili katika miongo sita.
KUMBUKA:- ziara ya  Mhe Rais Dkt  Samia Suluhu Hassan nchini China mwaka 2022 iliinua zaidi uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili kwani iliwafanya wananchi wa China kuona maeneo yanayofaa kwa uwekezaji nchini Tanzania na ziara anayoifanya Kati ya Septemba 2 hadi 6, 2024  inatarajia kuongeza zaidi chachu ya mafanikio baina ya nchi hizi mbili.