TSH BIL 21.7 ZAONGEZA NGUVU KWENYE UMWAGILIAJI
TANZANIA
Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetumia kiasi cha shilingi bilioni 21.7 kwa ajili ya ujenzi wa shamba la vitalu la Dkt Samia Suluhu Hassan, lililopo Mkoani Dodoma.
Mpango wa serikali katika mwaka wa fedha 2024/25 ni kuendelea kutekeleza miradi 780 ya umwagiliaji iliyoanza kutekelezwa mwaka wa fedha 2022/2023 na 2023/2024.
Aidha katika mwaka huu wa fedha tume ya Taifa ya umwagiliaji itafanya ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji katika skimu 33 zenye jumla ya hekta 6,089 ambazo zitawanufaisha wakulima 4,693.
Kukamilika kwa miradi ya ujenzi inayoendelea na inayotarajiwa kuanza mwaka 2024/2025 kutaongeza eneo la umwagiliaji kwa hekta 543,366.46 na kufanya jumla ya ardhi inayomwagiliwa kuwa hekta 1,270,647.06, ambayo ni asilimia 105.89 ya lengo la kufikia hekta 1,000 ifikapo mwaka 2025 kama ilivyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020.