HOSPITALI ZA RUFAA ZAFIKISHIWA TIBA MTANDAO
TANZANIA
Katika kuendelea kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya, Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya TEHAMA ikiwa ni pamoja na kuweka vifaa kama kompyuta na kamera katika vituo vya afya ili kuwezesha uanzishwaji wa huduma za tiba mtandao (Telemedicine).
Jumla ya hospitali za rufaa 16 na hospitali tatu za rufaa za kanda zimewekewa huduma ya tiba mtandao ambazo ni Iringa, Njombe, Mount Meru (Arusha), Manyara, Singida, Shinyanga, Simiyu, Mwalimu Nyerere Memorial (Musoma), Sekou Toure (Mwanza), Geita, Bukoba, Maweni (Kigoma), Kitete (Tabora), Ligula (Mtwara), Sumbawanga, Bombo (Tanga) Bugando, Benjamini Mkapa na Hospitali ya Kanda – Mbeya.
