SERIKALI KUJENGA NYUMBA 7,000
TANZANIA
Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Mashirika ya Nyumba imepanga kujenga jumla ya nyumba 7,000 za gharama ya kati na nafuu katika maeneo mbalimbali nchini.
Katika utekelezaji wa miradi hiyo, mradi wa Samia Housing Scheme unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa utajumuisha ujenzi wa nyumba 5,000 katika maeneo mbalimbali ambapo baadhi zimeshajengwa na kukamilika (Magomeni,Dar es Salaam) na mradi mwingine unaendelea kutekelezwa katika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam
