MASOKO, VITUO VYA MADINI VYAANZISHWA

 

MASOKO, VITUO VYA MADINI VYAANZISHWA

MASOKO, VITUO VYA MADINI VYAANZISHWA

DODOMA
Serikali imeanzisha jumla ya masoko 42 na vituo vya ununuzi wa madini 100 katika maeneo mbalimbali nchini ambapo thamani ya mauzo ya madini katika masoko na vituo vilivyoanzishwa yamefikia shilingi trilioni 1.74 na hivyo kuiwezesha Serikali kunufaika kwa kukusanya faida ya jumla ya shilingi bilioni 121.44. 
Aidha, Serikali imetoa jumla ya vibali 7,775 vya kuuza madini nje ya nchi yenye thamani ya shilingi trilioni 5.82.