WATOTO 14 WAWEKEWA VIFAA VYA USIKIVU

 

WATOTO 14 WAWEKEWA VIFAA VYA USIKIVU

WATOTO 14 WAWEKEWA VIFAA VYA USIKIVU

TANZANIA
Katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za ubingwa bobezi katika Hospitali ya Taifa, hospitali maalum na hospitali za kanda ikiwemo kuwawekea vifaa vya usikivu watoto 14.
Pia serikali kupitia wizara ya afya imefanikisha upandikizaji wa figo kwa wagonjwa 12, upasuaji wa moyo kwa njia ya tundu bila kufungua kifua na mishipa ya damu kwa wagonjwa 413, na wagonjwa wanne kufanyiwa upasuaji wa moyo kwa kupandikizwa mishipa bila kusimamisha moyo kwa mara ya kwanza kwa kutumia wataalam wa ndani.
Vilevile, wagonjwa 283 walifanyiwa upasuaji wa goti kwa kutumia matundu, wagonjwa 135 walifanyiwa upasuaji wa ubongo, jumla ya wagonjwa 166 wamewekewa puto tumboni tangu kuanzishwa na wagonjwa 19 wamefanyiwa upandikizaji uloto.