KATARYO KUJENGEWA SHULE MPYA YA SEKONDARI

 

KATARYO  KUJENGEWA SHULE MPYA  YA SEKONDARI

KATARYO  KUJENGEWA SHULE MPYA  YA SEKONDARI

MARA
Serikali ipo katika maandalizi ya kujenga shule mpya ya sekondari katika kijiji cha Kataryo  kilichopo katika Kata ya Tegeruka Jimbo la Musoma Vijijini,Mkoani Mara ili kukabiliana na changamoto ya masafa marefu ambayo wanafunzi wanakumbana nayo kwa sasa ya kutembea umbali wa takribani kilomita tano kufika shule ya sekondari iliyo karibu na Kijiji cha Tegeruka.
Mradi huo mpya pia unakusudiwa kuboresha miundombinu ya elimu ya sekondari, kuendana na mabadiliko katika mfumo wa elimu wa kitaifa na kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani.
Ujenzi wa shule hiyo mpya ya sekondari unatarajiwa kuanza hivi punde ili iweze kupokea wanafunzi mwezi Januari 2025 na itakapokamilika itaipatia Kata ya Tegeruka inayojumuisha vijiji vya Mayani, Kataryo na Tegeruka shule mbili za sekondari.