“HATUJAVAMIA NCHI YOYOTE NA HATUNA MPANGO HUO” DKT SAMIA
DAR ES SALAAM
AMIRI Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa miaka 60 limefanya kazi kikamilifu na kwa ufanisi mkubwa.
Dkt Samia ametoa kauli hiyo Septemba Mosi 2024 wakati akishiriki kilele cha miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dares salaam.
Amesema”jeshi letu limeendelea kuwa ni jeshi la ulinzi na sio jeshi la uvamizi,hatujavamia nchi yoyote na hatuna mpango huo”
Dkt Samia ameongeza kwamba “ jeshi letu limekuwa jeshi la ukombozi,na kioo katika harakati za ukombozi wa Afrika na kulinda amani Duniani, hongereni makamanda na wapiganaji”
Halikadhali Dkt Samia ametumia maadhimisho hayo kuwasihi wananchi wa Tanzania kuendelea kutimiza wajibu wa kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 28 (1) kulinda nchi yetu na kuwakemea wanaochochea uhasama na uvunjifu wa amani ndani ya nchi yetu.