FAHAMU KUHUSU IDADI YA SHULE (AWALI-SEKONDARI)
TANZANIA
Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI inaratibu usimamizi na uendeshaji wa elimu ya awali, msingi na sekondari nchini kupitia mamlaka za serikali za mitaa.
Kwa kusimamia vema eneo lake la utekelezaji, hadi kufikia mwezi Machi, 2024 idadi ya shule zenye madarasa ya awali ni 20,316 (17,942 za Serikali na 2,374 zisizo za Serikali), idadi ya shule za msingi 20,384 (17,986 za Serikali na 2,398 zisizo za Serikali) zikiwemo shule maalumu za msingi 37 za bweni na vitengo maalumu 710.
Aidha, idadi ya shule za sekondari ni 6,263 (4,894 za Serikali na 1,369 zisizo za Serikali).