2023/24 TAMISEMI ILIIDHINISHIWA TSH TRILIONI 9.18 (UALIMU)
TANZANIA
Katika mwaka wa fedha 2023/24 Ofisi ya Rais - TAMISEMI Fungu Namba 56, Tume ya Utumishi wa Walimu Fungu Namba 02 na Mafungu 26 ya mikoa yakijumuisha halmashauri 184 yaliidhinishiwa bajeti ya shilingi trilioni 9.18.
Kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 3.52 ni Fedha za Maendeleo na shilingi trilioni 5.65 ni za Matumizi ya Kawaida, yakijumuisha Mishahara shilingi trilioni 4.59 na matumizi Mengineyo ni shilingi trilioni 1.06.