TSH MIL 638 ZAJENGA SHULE MTIMBWILIMBWI
MTWARA.
Serikali imepeleka fedha kiasi cha shilingi milioni 638 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari kidato cha tano na sita katika kata ya Mtimbwilimbwi Halmashauri ya Mji Nanyamba, Mkoani Mtwara.
Kiasi hicho cha fedha kimefanikiwa kujenga madarasa nane, mabweni matatu na matundu ya vyoo 16, Ujenzi umeanza mwezi wa tano na unatarajiwa kukamilika mwezi huu (Septemba) 2024.