VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA YA AFYA MSINGI VYAFIKIA 1,663
TANZANIA
Takwimu zinaonesha kuna ongezeko la vituo vya afya ya msingi 1,663 ikilinganishwa na idadi ya vituo 5,270 vilivyokuwepo mwaka 2015 wakati wa mkakati wa kuboresha na kuanza ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya.
Aidha serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI inasimamia vituo vya kutolea huduma za afya ya msingi 6,933 ambapo zahanati ni 5,887, vituo vya afya 874 na hospitali za halmashauri 172.